The next generation of African architects and designers | Christian Benimana

85,649 views ・ 2018-01-19

TED


Tafadhali bofya mara mbili manukuu ya Kiingereza hapa chini ili kucheza video.

Translator: Neria-Neema Kwayu Reviewer: Julieth Mbeyella
00:12
The longest journey that I have ever taken.
0
12780
2871
Safari ndefu ambayo nimewahi kusafiri,
00:16
That was in 2002.
1
16470
1844
Ilikuwa ni mwaka 2002
00:18
I was only 19 years old.
2
18869
1429
Nilikuwa na miaka 19
00:21
It was the first time I had ever been on an airplane
3
21146
3329
Ilikuwa ni mara ya kwanza kupanda ndege
00:24
and the first time that I had left my country,
4
24499
2805
na mara ya kwanza kutoka nje ya nchi.
00:27
Rwanda.
5
27328
1150
Rwanda,
00:29
I had to move thousands of kilometers away
6
29423
3191
Ilibidi niende umbali wa maelfu ya kilometa
00:32
to follow a dream.
7
32638
1280
kufwata ndoto zangu.
00:34
A dream I have had ever since I was a child.
8
34262
3012
Ndoto niliyokuwa nayo tangu utotoni,
00:37
And that dream was to become an architect.
9
37889
3973
Na hiyo ndoto ilikuwa ni kuwa msanifu majengo.
00:43
That was impossible at the time in my country.
10
43264
2601
Kipindi hicho ilikuwa haiwezekani nchini mwangu.
00:45
There were no schools of architecture.
11
45889
1831
Kulikuwa hamna shule za usanifu majengo.
00:48
So when I got a scholarship to study in China,
12
48426
3061
Kwahiyo nilivyopata msaada wa kwenda kusoma china,
00:51
I left my life and my family behind
13
51511
2706
niliacha maisha yangu na familia nyuma
00:54
and I moved to Shanghai.
14
54241
1841
nikahamia Shanghai.
00:56
It was an amazing time.
15
56724
2017
Ilikuwa ni wakati mzuri
00:59
This country was going through a major building boom.
16
59252
4327
Nchi ilikuwa inapitia mlipuko wa majengo.
01:03
Shanghai, my new home,
17
63603
1783
Shanghai nyumbani kwangu kupya
01:05
was quickly turning into a skyscraper city.
18
65410
2542
ilikuwa inabadilika kuwa mji wenye maghorofa mengi.
01:09
China was changing.
19
69241
1694
China ilikuwa inabadilika
01:10
World-class projects were built to convey a new image of development.
20
70959
4436
Mipango mji mipya ilijengwa ili kuleta muonekano mpya wa maendeleo.
01:15
Modern, striking engineering marvels were going up literally everywhere.
21
75889
5690
Majengo mapya ya kustaajabisha yalikuwa yanajengwa kila sehemu,
01:22
But behind these facades,
22
82493
2695
Lakini nyuma ya hii yote,
01:25
exploitation of huge numbers of migrant workers,
23
85212
4222
utumikwishaji wa wafanyakazi wengi wa kigeni,
01:29
massive displacement of thousands of people
24
89458
3157
utenganeshwaji wa maelfu ya watu
01:32
made these projects possible.
25
92639
2023
uliifanya hii miradi ifanikiwe.
01:35
And this fast-paced development
26
95042
1926
Na haya maendeleo ya haraka
01:36
also contributed significantly to the pollution
27
96992
2987
yalichangia kuchafua mazingira kwa kiasi kikubwa.
01:40
that is haunting China today.
28
100003
1636
amabayo ina hatarisha China leo.
01:42
Fast-forward to 2010,
29
102758
1938
Mnamo mwaka 2010
01:44
when I went back home to Rwanda.
30
104720
2128
nilivyorudi nyumbani Rwanda
01:47
There, I found development patterns similar to what I saw in China.
31
107320
4252
Kule, nikakuta maendeleo yanayofanina na China.
01:52
The country was and still is experiencing its own population and economic growth.
32
112087
5972
Nchi ilikuwa na bado ina pitia ukuaji wake wa kiuchumi na kijamii,.
01:58
The pressure to build cities, infrastructure and buildings
33
118574
3175
Msukumo wa kujenga miji , miundombini na majengo.
02:01
is at its peak,
34
121773
1896
upo kwenye ukubwa wake
02:03
and as a result,
35
123693
1222
na matokeo yake,
02:04
there is a massive building boom as well.
36
124939
2404
kuna mlipuko wa majengo pia.
02:08
This is the reality across the entire continent of Africa,
37
128392
4874
Huu ndo uhalisia ulioko kwenye bara zima la Africa,
02:13
and here's why.
38
133290
1150
Na hii ndo sababu.
02:14
By 2050, Africa's population will double,
39
134913
3108
Ifikapo mwaka 2050, idadi ya watu Africa itakuwa mara mbili.
02:18
reaching 2.5 billion people.
40
138045
3487
Kufikia watu billioni 2.5.
02:22
At this point,
41
142323
1612
Ifikapo hapo
02:23
the African population will be slightly less than the current population
42
143959
5031
Idadi ya watu wa Africa itakuwa pungufu kidogo kuzidi ilivyo sasa
02:29
of China and India combined.
43
149014
4142
ya China na India.
02:34
The infrastructure and buildings needed to accommodate this many people
44
154963
4969
Miundombinu na majengo yanayohitajika kuhimili watu wengi kiasi hiki
02:39
is unprecedented in the history of humankind.
45
159956
3535
haijategemewa kwenye historia ya binadamu.
02:44
We have estimated that by 2050,
46
164072
3338
Tumekisia kwamba ifikapo mwaka 2050
02:47
we have to build 700,000,000 more housing units,
47
167434
5218
inabidi tujenge zaidi ya nyumba 700,000,000
02:52
more than 300,000 schools
48
172676
2988
shule takribani 300,000
02:55
and nearly 100,000 health centers.
49
175688
3989
na sehemu za huduma za kiafya zisizopungua 100,000.
03:01
Let me put that into perspective for you.
50
181173
2667
Ngoja nikupe muelekeo
03:04
Every day for the next 35 years,
51
184902
3682
Kila siku kwa miaka 35 ijayo
03:08
we have to build seven health centers,
52
188608
2913
inabidi tujenge sehemu saba za huduma za afya.
03:11
25 schools
53
191545
1858
shule 25
03:13
and nearly 60,000 housing units each day,
54
193427
4702
na karibia uniti 60000 za nyumba kila siku,
03:18
every day.
55
198153
1290
kila siku
03:22
How are we going to build all of this?
56
202039
2872
Tutawezaje kujenga hivi vyote?
03:25
Are we going to follow a model of unsustainable building and construction
57
205698
4357
Je tutafwata mfano wa ujenzi usio salama
03:30
similar to what I witnessed in China?
58
210079
2216
kama ule wa China?
03:32
Or can we develop a uniquely African model
59
212319
4033
Au tutaweza kutengeneza wa kwetu wa kipekee wa Africa.
03:36
of sustainable and equitable development?
60
216376
3072
Ambao utakuwa wa kuridhisha na wa faida kwa maendeleo?
03:39
I'm optimistic we can.
61
219905
1689
Nina amini tunaweza.
03:41
I know Africans who are already doing it.
62
221992
2568
Nawajua Wa Africa ambao tayari wanaufanya.
03:45
Take Nigerian architect Kunlé Adeyemi for instance,
63
225334
3040
Mfano msanifu majengo wa Nigeria Kunlé Adeyemi,
03:48
and his work in slums of coastal megacities.
64
228398
3237
Na kazi zake kwenye mitaa ya Pwani za miji mikubwa.
03:52
Places like Makoko in Lagos,
65
232121
2921
Sehemu kama Makoko Lagos
03:55
where hundreds of thousands of people live in makeshift structures on stilts
66
235066
4761
Ambapo mamia maelfu ya watu wanaishi kwenye vijijumba vya kushona
03:59
on water,
67
239851
1177
vilivyo juu ya maji,
04:01
without government infrastructure or services.
68
241052
2407
bila miundo mbinu ya serikali wala huduma za kijamii.
04:04
A community at great risk of rising sea levels and climate change.
69
244272
5570
Jamii iliyo katika hatari ya muongezeko wa maji na mabadiliko ya tabia nchi.
04:10
And yet, people who live here are examples of great ingenuity
70
250223
4353
Lakini bado watu wanaoishi hapo ni mfano wa wapambanaji
04:14
and the will to survive.
71
254600
2021
na wenye nia ya kuishi.
04:16
Kunlé and his team have designed a prototype school
72
256645
3075
Kunlé na timu yake wametengeneza shule ya mifano.
04:19
that is resilient to rising sea levels.
73
259744
2969
Ambayo inavumilia maji ya bahari yanyoongezeka.
04:22
This is Makoko School.
74
262737
2252
Hii ni shule ya Makoko.
04:26
It's a floating prototype structure that can be adapted to clinics,
75
266502
4205
Ni mfano wa jengo linaloeleya ambalo linaweza kutumika kwenye kliniki,
04:30
to housing, to markets
76
270731
2749
nyumba na masoko
04:33
and other vital infrastructure this community needs.
77
273504
2548
na miundombinu mingine ambayo hii jamii inahitaji.
04:36
It's an ingenious solution
78
276076
2040
Ni moja la jibu la kipekee
04:38
that can ensure this community lives safely on the waters of Lagos.
79
278140
4754
amabalo linaweza hakikisha maisha ya hii jamii ambayo inaishi kwenye maji ya Lagos.
04:43
This is Francis Kéré.
80
283895
2055
Huyu ni Francis Kéré.
04:46
He works in the country where he comes from,
81
286726
2049
Anafanya kazi kwenye nchi anayotokea.
04:48
Burkina Faso.
82
288799
1150
Burkina Faso.
04:50
Kéré and his team have designed projects that use traditional building techniques.
83
290374
5556
Kéré na timu yake wametengeneza miradi ambayo inatumia njia za kitamaduni za ujenzi.
04:56
Kéré and his team working in the communities
84
296434
2655
Kéré na timu yake wanafanya kazi kwenye jamii
04:59
have developed prototype schools
85
299113
2821
na wametengeneza shule za mifano
05:01
that the whole community,
86
301958
1492
ambazo jamii nzima.
05:03
similar to every project in the villages of this country,
87
303474
3624
zinafanana na kila mradi kwenye vijiji vya nchi hii
05:07
comes together to build.
88
307122
1888
inakuja pamoja kujenga.
05:10
Children bring stones for the foundation,
89
310028
2983
Watoto wanaleta mawe kwa ajili ya msingi,
05:13
women bring water for the brick manufacturing,
90
313035
3331
wanawake wanaleta maji kwa ajili ya upauaji wa matofali,
05:16
and everybody works together to pound the clay floors.
91
316390
3652
na kila mtu anafanya kazi kubonda sakafu za udongo
05:20
Working with the community,
92
320946
1286
pamoja na jamii,
05:22
Kéré and his team have created projects that function better,
93
322256
3635
Kéré na timu yake wametengeneza miradi inayofanya kazi vizuri
05:25
with adequate lighting and adequate ventilation.
94
325915
2636
kwa mwanga na uingizaji hewa wa kutosha.
05:29
They're appropriate for this particular context
95
329231
3072
Zinafaa kwenye huu mstakabali
05:32
and really, really beautiful as well.
96
332327
1826
na ni nzuri mno mno.
05:34
For the past seven years,
97
334881
1763
Kwa miaka saba iliyopita,
05:36
I have been working as an architect at MASS Design Group.
98
336668
3574
nimekuwa nikifanya kazi kama msanifu majengo wa MASS Design Group.
05:40
It's a design firm that began in Rwanda.
99
340266
2717
Ni kampuni ya ubunifu iliyoanzishwa Rwanda.
05:44
We have worked in several countries in Africa,
100
344480
3230
Tumefanya kazi na nchi nyingi Africa,
05:47
focusing on this more equitable and sustainable model
101
347734
4313
Tukilenga huu mpango wa kukidhi na wenye faida,
05:52
of architectural practice,
102
352071
1840
wa usanifu majengo.
05:53
and Malawi is one of those countries.
103
353935
2220
Na Malawi ni moja ya hizo nchi.
05:56
It's a country with beautiful, remote landscapes
104
356587
3404
Ni nchi yenye mazingira mazuri yaliyojificha.
06:00
with high-peak mountains and fertile valleys.
105
360015
2973
yenye milima yenye vilele virefu na ardhi yenye rutuba.
06:03
But it also has one of the worst maternal mortality rates in the world.
106
363440
4015
Lakini pia ina idadi kubwa za vifo vya kina mama duniani.
06:09
A pregnant woman in Malawi either gives birth at home,
107
369067
3477
Mwanamke mwenye mimba Malawi huzalia nyumbani au
06:12
or she has to walk a really long journey to the nearest clinic.
108
372568
3986
hutembea safari ndefu kuelekea kliniki ya karibu.
06:17
And one out of 36 of these mothers dies during childbirth.
109
377535
5439
Na moja kati ya kina mama 36 anafariki wakati wakujifungua.
06:24
In Malawi,
110
384647
1151
Malawi
06:25
with our team at MASS Design Group,
111
385822
1890
na timu yetu ya MASS Design Group
06:27
we designed the Kasungu Maternity Waiting Village.
112
387736
2410
Tumetengeneza kijij cha kina mama cha kusubiria kujifungua.
06:30
This is a place women come to six weeks before their due dates.
113
390856
4013
Hii ni sehemu ambayo wanawake wanakuja wiki 6 kabla ya kujifungua.
06:35
Here they receive prenatal care
114
395733
1858
Hapa wanapata matunzo ya uzazi
06:37
and train in nutrition and family planning.
115
397615
3436
na kujifunza kuhusu lishe na uzazi wa mpango.
06:41
At the same time, they form a community
116
401604
2568
Wakati huo huo wanatengeneza umoja
06:44
with other expectant mothers and their families.
117
404196
2519
na wakina mama wengine wanaosubiria kujifungua na familia zao.
06:48
The design of the of Kasungu Maternity Waiting Village
118
408960
2525
Muundo wa kijiji cha kusubiria kujifungulia cha Kasungu
06:51
borrows from the vernacular typologies of Malawi villages
119
411509
4104
inaazima ukienyeji wa vijiji vya Malawi
06:55
and is built using really simple materials and techniques.
120
415637
4203
na imejengwa kutumia nyenzo na mbinu rahisi .
07:00
The earth blocks that we used were made from the same soil of this site.
121
420230
4785
Matofali tunayotumia yametengenezwa na udongo wa kwenye eneo hili hili
07:05
This reduces the carbon footprint of this building,
122
425803
3293
Hii inapunguza matumizi ya cabon kwenye jengo hili,
07:09
but first and foremost,
123
429120
2071
lakini kabla ya yote.
07:11
it provides a safe and dignified space for these expectant mothers.
124
431215
5627
Inaleta sehemu safi na inayofaa kwa ajili ya akina mama.
07:17
These examples show that architecture and design
125
437361
2944
Hii mifano inaonesha kuwa majengo na miundo
07:20
have the power and the agency to address complex problems.
126
440329
5931
ina nguvu na uwezo wa kutatua matatizo yanayotukabiri.
07:27
But more to point,
127
447885
2732
Lakini la umuhimu zaidi
07:30
that we can develop a model of effective solutions
128
450641
3697
tunaweza tengeneza mifano ya kutatua matatizo
07:34
for our communities.
129
454362
1379
kwenye jamii zetu.
07:36
But these three examples are not enough.
130
456476
2540
Lakini mifano hii mitatu haitoshi
07:40
300 more examples will not be enough.
131
460128
3230
Mifano mingine 300 haitotosha.
07:44
We need a whole community of African architects and designers
132
464198
5358
Tunahitaji jamii nzima ya waasnifu majengo na wabunifu wa ki Afrika.
07:49
to lead with thousands more examples.
133
469580
2923
Waongoze kwa mifano mingi zaidi
07:53
In May of this year,
134
473182
1842
Mnamo Mei mwaka huu
07:55
we convened a symposium on African architecture, in Kigali,
135
475048
3571
tulifanya mkutano wa wasanifu majengo wa Africa, Kigali,
07:58
and we invited many of the leading African designers
136
478643
3698
na tukawaalika wabunifu wengi wa Africa
08:02
and architectural educators working across the continent.
137
482365
3619
na waalimu wa usanifu majengo wanaofanya kazi ndani ya bara hili
08:06
We all had one thing in common.
138
486617
2049
Sote tulikuwa na jambo moja la kufanana
08:10
Every single one of us went to school abroad
139
490398
4167
Sote tulisoma shule ulaya
08:14
and outside of Africa.
140
494589
1881
na nje ya Africa
08:16
This has to change.
141
496494
1587
Hii inabidi ibadilike.
08:19
If we are to develop solutions unique to us,
142
499271
3357
Kama tunataka kutengeneza mipango inayoendana na sisi
08:22
rather than attempting to turn Kigali into Beijing,
143
502652
3476
kulikoni kutaka kuibadilisha Kigali iwe Beijing
08:26
or Lagos into Shenzhen,
144
506152
2485
au Lagos iwe Shenzen
08:28
we need a community
145
508661
1754
tunahitaji jamii
08:30
that will build the design confidence of the next generation
146
510439
3325
itakayojenga miundo ya kujiamini ya jamii inayokuja
08:33
of African architects and designers.
147
513788
2378
ya wasanifu majengo na wabunifu wa ki Africa.
08:36
(Applause)
148
516846
7470
(Makofi)
08:44
In September last year,
149
524719
1312
Mnamo September mwaka jana,
08:46
we launched the African Design Centre
150
526055
3080
tulianzisha kituo cha ubunifu cha Africa
08:49
to start building this community.
151
529159
2705
tuanze kujenga hii jamii
08:53
We admitted 11 fellows from across the continent.
152
533700
3217
Tuliwaweka wanafunzi 11 kutoka kwenye bara zima.
08:58
It's a 20-month-long, design-build fellowship program.
153
538021
4338
Ni kozi inayodumu kwa miezi 20
09:03
Here, they are learning to tackle big challenges
154
543091
2890
Hapa wanajifunza kukabiliana na vikwazo vikubwa
09:06
such as urbanism and climate change,
155
546005
2512
kama mabadiliko ya tabia hewa na mipango miji
09:08
as Kunlé and his team have.
156
548541
1779
kama ambavyo Kunlé na timu yake wamefanya.
09:11
They're working with communities
157
551367
1583
Wanafanya kazi na jamii
09:12
to develop innovative building solutions and processes,
158
552974
4084
kuendeleza mipango ya ujenzi na miundo mbinu
09:17
as Kéré and his team have.
159
557082
2205
kama ambavyo Kéré na timu yake wamefanya.
09:20
They're learning to understand the health impact of better buildings
160
560230
4001
Wanajifunza kuelewa umuhimu wa kiafya wa majengo mazuri
09:24
as we at MASS Design Group have been researching
161
564255
3476
kama ambavyo sisi wa MASS Design Group tumekuwa tukifanya uchunguzi
09:27
for the past several years.
162
567755
1606
kwa miaka kadhaa iliyopita.
09:29
The crowning moment of the fellowship
163
569896
2312
Muda wa sifa wa huu ushirika
09:32
is a real project that they designed and built.
164
572232
3643
ni mradi walio sanifu na kujenga.
09:36
This is Ruhehe Primary School,
165
576407
2517
Hii ni shule ya msingi ya Ruhehe,
09:38
the project they designed.
166
578948
1459
mradi walio usanifu.
09:40
They immersed themselves in the community to understand the challenges
167
580431
4303
Walijikita kwenye jamii ili waelewe matatizo yanayoikabili.
09:44
but also uncover opportunities,
168
584758
2305
Lakini pia kuzindua njia mpya,
09:47
like using a wall made of local volcanic stone
169
587087
4132
kama vile kutumia ukuta uliotengenezwa na mawe ya volkano.
09:51
to turn the entire campus into a space of play and active learning.
170
591243
4077
kubadilisha mazingira mazima ya chuo kuwa sehemu ya kucheza na kujifunza.
09:56
They evaluated the environmental conditions
171
596644
2846
Walitathimini hali ya mazingira,
09:59
and developed a roof system that maximizes daylight
172
599514
3254
na kutengeneza mfumo wa paa ambao unaongeza mwanga wa jua
10:02
and improves acoustic performance.
173
602792
2058
na unaongeza utendaji wa sauti.
10:05
The construction at Ruhehe Primary School will begin this year.
174
605243
4190
Ujenzi wa shule ya msingi ya Ruhehe utaanza mwaka huu.
10:10
(Applause)
175
610861
5874
(Makofi)
10:16
And over the coming months,
176
616759
1484
Na kwenye miezi inayofuatia
10:18
the African Design Centre fellows are going to work hand-in-hand
177
618267
3606
wasomi wa chuo cha ubunifu cha Afrika watafanya kazi moja kwa moja
10:21
with the Ruhehe community to build it.
178
621897
2537
na jamii ya Ruhehe kuijenga.
10:25
When we asked the fellows
179
625493
1243
Tulivyowauliza wanafunzi
10:26
what they want to do after their African Design Centre fellowship,
180
626760
3792
wanataka kufanya nini baada ya kukamilisha fellowshipu yao ya Ubunufu wa kiAfrica,
10:30
Tshepo from South Africa said
181
630576
2259
Tsepo kutoka South Africa alisema,
10:32
he wants to introduce this new way of building into his country,
182
632859
3255
anataka kutambulisha hii namna mpya ya kujenga nchini kwake.
10:36
so he plans to open a private practice in Johannesburg.
183
636138
3245
Kwa hivyo ana mpango wa kufungua kampuni yake binafsi Johannesburg,
10:39
Zani wants to expand opportunities for women to become engineers.
184
639985
4253
Zani anataka kutanua nafasi kwa wanawake wawe wahandisi.
10:44
Before joining the African Design Centre,
185
644966
2136
kabla ya kujiunga na kituo cha Ubunifu cha Afrika.
10:47
she helped start, in Nairobi,
186
647126
1732
alisaidia kuanzisha, Nairobi,
10:48
an organization to bridge the gender gaps for women in engineering fields,
187
648882
4691
shirika la kusaidia kuziba pengo la wanawake kwenye sekta ya uhandisi,
10:53
and she hopes to take this movement across Africa,
188
653597
3250
na anategemea kupeleka huu msimamo Afrika nzima.
10:56
eventually the whole world.
189
656871
1577
mwishowe dunia nzima.
10:59
Moses, from South Sudan,
190
659574
2443
Moses kutoka sudan ya kusini
11:02
the world's newest country,
191
662041
2175
nchi mpya duniani
11:04
wants to open the first polytechnic school
192
664240
2992
anataka kufungua shule mpya ya ufundi wa teknolojia.
11:07
that will teach people how to build using local materials from his country.
193
667256
5024
ambayo itafundisha watu ujenzi kwa kutumia malighafi zilizoko nchini mwao
11:13
Moses had to be determined to become an architect.
194
673746
3498
Moses alitamani kuwa msanifu majengo.
11:18
The civil war in his country frequently interrupted his architectural education.
195
678105
5312
Vita za wenyewe kwa wenyewe nchini kwao ziliingilia masomo yake.
11:24
At the time he was applying to join the African Design Centre,
196
684430
3356
Wakati anajiaandaa kuanza kusoma kwenye kituo cha Ubunifu cha Afrika
11:27
we could hear gunshots going off in the background of his interview call.
197
687810
4691
tulikuwa tunasikia bunduki zikilia nyuma ya simu yake ya mahojiano.
11:33
But even in the middle of this civil war,
198
693546
3326
Lakini katikati ya vita ya wenyewe kwa wenyewe
11:36
Moses hangs on to this idea
199
696896
1835
Moses alishikilia wazo lake
11:38
that architecture can be a way to bridge communities back together.
200
698755
5026
la kwamba usanifu majengo unaweza kuwa njia ya kufanya jamii ziwe pamoja.
11:44
You have to be inspired by this fellow's belief
201
704727
3310
Imani za mwanafunzi huyu zinatoa msukumo
11:48
that great architecture can make a difference
202
708061
2524
wa kwamba usanifu majengo unaleta tofauti,
11:50
on how the future of Africa is built.
203
710609
2810
wa jinsi ambavyo Afrika inajengwa.
11:54
The unprecedented growth of Africa cannot be ignored.
204
714514
3756
Ukuaji wa Afrika hauwezi kusahauliwa
11:59
Imagine Africa's future cities,
205
719258
3623
Waza miji mipya ya Afrika,
12:02
but not as vast slums,
206
722905
2482
lakini sio kama makazi duni
12:05
but the most resilient
207
725411
1881
lakini zenye uvumulivu
12:07
and the most socially inclusive places on earth.
208
727316
3381
na zenye jamii za kushabihiana zaidi duniani.
12:10
This is achievable.
209
730721
2127
Hili linawezekana
12:13
And we have the talent to make it a reality.
210
733909
4119
Na tuna uwezo wa kulifanya litokee.
12:18
But the journey to ready that talent for the task ahead,
211
738052
3987
Lakini safari ya kuandaa vipaji vya yajayo mbeleni
12:22
like my own journey,
212
742063
1667
kama safari yangu,
12:23
is far too long.
213
743754
1246
ni ndefu sana.
12:26
For the next generation of African creative leaders,
214
746674
4433
Kwa vizazi vijavyo vya wabunifu wa Ki Africa
12:31
we have to shorten and streamline that journey.
215
751131
3435
inabidi tufupishe hii safari.
12:35
But most importantly --
216
755106
1386
Lakini la umuhimu zaidi--
12:36
and I cannot stress this enough --
217
756516
2323
na siwezi kuliwekea msisitizo wa kutosha--
12:38
we have to build their design confidence
218
758863
2278
tunahitaji kujenga kujiamini kwao kiubunifu
12:41
and empower them to develop solutions that are truly African
219
761165
4193
na kuwapa nguvu kutengeneza majibu ya ki Africa
12:45
but globally inspiring.
220
765382
2211
lakini yafae kwa dunia nzima.
12:48
Thank you very much.
221
768082
1151
Asante sana.
12:49
(Applause)
222
769257
7000
(Makofi)
Kuhusu tovuti hii

Tovuti hii itakuletea video za YouTube ambazo ni muhimu kwa kujifunza Kiingereza. Utaona masomo ya Kiingereza yanayofundishwa na walimu wa kiwango cha juu kutoka duniani kote. Bofya mara mbili kwenye manukuu ya Kiingereza yanayoonyeshwa kwenye kila ukurasa wa video ili kucheza video kutoka hapo. Manukuu yanasonga katika kusawazishwa na uchezaji wa video. Ikiwa una maoni au maombi yoyote, tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia fomu hii ya mawasiliano.

https://forms.gle/WvT1wiN1qDtmnspy7